Blog

Nini hutokea ndani ya uwanja, usichokijua.

Sambaza....

Katika football kuna mpango wa mchezaji moja moja (individually) kuna mpango wa group madogo madogo miongoni mwa idara za uwanjani kama Walinzi,Viungo na Washambuliaji.

Lakini kuna mpango wa ujumla huu lazima utoke kwenye benchi la ufundi ( Game Plan au match strategic) na waweza kusema ni filosofi ya Kochainapoanza kufanya kazi.

Tafiti inaonesha kama kuna uhusiano bora / urafiki mkubwa baina ya wachezaji ndani ya timu yumkini wakatengeneza mpango wao lengo likiwa kupata ushindi.

Kwa mfano kwa sasa PSG ya sasa washambuliaji wake wamewaka, Neymar Mbappe na Messi hii inaweza ikawa inachangiwa na ushikaji wao.

Football ni pana haishii kwenye eneo la kucheza tu ,ushindi kwenye soka unachangiwa na vitu vingi sana lakini mahusiano bora ( umoja ) ni moja ya silaha kubwa sana.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.