Ligi Kuu

Nitaacha wachezaji 19- Zahera

Sambaza....

Harakati za usajili katika klabu ya Yanga zinaendelea kwa kasi kubwa, baada ya msimu uliomalizika kuwa na kikosi hafifu Yanga wanapigana ili wawe na kikosi ambacho ni imara.

Kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera amedai kuwa kwa sasa anaendelea kusajili wachezaji ambao anaona wanaweza kuisaidia timu.

“Kabla sijaenda kwenye kambi ya timu ya taifa nitasajili wachezaji wanne ambao tutakuwa nao msimu ujao”. Alisema Mwinyi Zahera.

Yanga wakishangilia

Kuhusu idadi ya wachezaji atakaowaacha kwa ajili ya msimu ujao amedai kuwa kuna idadi kubwa ya wachezaji ambao hawana mkataba kwa sasa.

” Kuna wachezaji zaidi ya 19 ambao mikataba yao imeisha mpaka sasa hivi, kwa hiyo nikiamka kesho nikawaza kuwaacha nitawaacha”- alidai kocha huyo kutoka Congo.

Kuhusu sehemu ambayo Yanga itaenda kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu msimu ujao, Kocha Huyo amedai wataenda China.

“Naenda kwenye majukumu ya timu ya taifa, ila timu yangu itaenda China kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao”- alisema kocha huyo wa Yanga.


Wachezaji gani ungependa kuwaona tena msimu ujao? Tupe maoni hapo chini


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.