Niyonzima wakati wa mchezo wa Samatta vs Alikiba
Ligi

Niyonzima kutua leo kwa ajili ya kuiua Simba

Sambaza....

Dirisha dogo la usajili msimu huu lilifunguliwa na Yanga walihakikisha wanaanza kujiimarisha sehemu ambazo waliona wao kama wao wana mapungufu kwa kiasi kikubwa.

Kwenye dirisha dogo walifanikiwa kumsajili Tariq Seif , Ditram Nchimbi, Yikpe Domminick mchezaji kutoka Ivory Coast na kumrejesha kundini Haruna Niyonzima.

Tariq Seif akiwa katika jezi ya Biashara utd msimu uliopita!

Huyu aliwahi kuichezea Yanga na kuwa kipenzi kikubwa cha mashabiki wa Yanga , lakini msimu juzi alienda kwa mahasimu wao wakubwa Simba lakini mkataba ulipoisha alirudi nyumbani kwao kucheza Kigali FC.

Kwenye dirisha hili dogo amerejeshwa tena , na swali kubwa lililokuwa linazunguka ni lini atafika nchini kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho cha mabingwa wa kihistoria. Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amedhibitisha kuwa Leo Haruna Niyonzima atatua rasmi Mchana kwa ajili ya kuwakabili Simba.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.