Niyonzima
Ligi Kuu

Niyonzima ndiye mchezaji mwenye akili Yanga- KOCHA WA YANGA

Sambaza....

 

Jana Yanga wametoka suluhu na Tanzania Prisons na inakuwa mechi ya pili mfululizo kuchukua alama moja baada ya kutoka sare ya (1-1) dhidi ya Mbeya City mechi iliyopita iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa pia.

Baada ya mchezo huo kocha wa Yanga alizungumza na vyombo vya habari ikiwemo Kandanda.co.tz iliyoshuhudia mchezo huo wa jana .

Kocha huyo alidai kuwa katika mechi ya jana alikosa akili ya Haruna Niyonzima pamoja na kufanya mabadiliko ya wachezaji tofauti tofauti katika mechi ya jana .

“Haruna Niyonzima ni mgonjwa anaumwa Malaria ndiyo maana katika mchezo wa Leo hatukuweza kuwa naye “-alisema kocha huyo mkuu wa Yanga .

Kocha huyo aliongezea kuwa kwenye timu ya Yanga ilikosekana akili ya Haruna Niyonzima ambaye alikuwa anaumwa katika mechi ya Jana .

“Timu ilikosa akili ya Haruna Niyonzima katika mechi ya Jana , na kwa bahati mbaya alikuwa anaumwa Malaria ndiyo maana hajacheza “- alimalizia kocha huyo.

Ditram Nchimbi “Duma” akiwa mazoezini na klabu yake ya Yanga.

Yanga katika mechi mbili zilizopita wamefanikiwa kupata alama mbili na wanaenda Moshi kwa ajili ya kucheza na Polisi Tanzania jumanne hii katika uwanja wa ushirika Moshi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.