ASFC

Nyuki wa ‘SIMBA’ wawavamia YANGA

Sambaza....

Leo katika mchezo wa kombe la shirikisho Tanzania maarafu kama kombe la Chama cha soka nchini (TFF) Kati ya Yanga FC na Iringa FC kulitokea tukio la ajabu Baada ya nyuki kuvamia wakati mechi inaendelea.

Tukio hilo lilisababisha mchezo huo kusimama kwa muda , nyuki wale walihusishwa na imani za kishirikina na baadhi ya mashabiki hasa hasa mashabiki wa Yanga.

Mashabiki hao wanaamini kabisa nyuki wale walitumwa na mahasimu wao nchini Simba kwa ajili ya kuwadhoofisha kwenye mechi ijayo itakayochezwa tarehe 4mwezi wa kwanza mwakani.

“Hawa ni nyuki wa Simba wamewatuma kwa makusudi ili tu kutudhoofisha kwenye mechi yetu na wao “- alisikika shabiki mmoja aliyekuwa amekaa jukwaani.

“Baada ya kuona tunafanya usajili  wameanza kuwa na hofu kubwa ndiyo maana wametuma nyuki”- alisikika shabiki mwingine wa Yanga.

“Wameona Hakuna njia nyingine ya kutufunga zaidi ya wao kutuma nyuki , na kwa taarifa Yao wameshindwa wajiandae kwa ajili ya kipigo”. Vituko hivo vinaendelea kuelekea kwenye mechi hiyo kubwa Afrika nzima.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.