Sambaza....

Mshambuliaji wa timu ya Majimaji, Marcel Kaheza amechaguliwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom mwezi Aprili.

Kaheza atapewa fedha milioni moja na wadhamini wakuu wa ligi Kampuni ya Vodacom, kisimbuzi cha Azam TV

Kaheza amewapiku washambuliaji nyota wa timu ya Simba, John Bocco na Emmanuel Okwi kwenye kinyang’anyiro hicho.

 

Katika mwezi huo Kaheza amefunga mabao saba yakiwemo matatu ‘hat trick’ katika mchezo mmoja.
dhidi ya Ruvu Shooting vile vile ameiwezesha Majimaji kutoka mkiani mwa msimamo mwezi Machi hadi nafasi ya 14 sasa.

Katika mwezi uliopita Emmanuel Okwi alifunga magoli 3 na kutoa pasi za mwisho 2 wakati John Bocco akifunga magoli manne (4) na kutoa pasi mbili za mwisho za magoli.

Sambaza....