Kagere
Blog

Pamoja na ‘Uzee’ wa Kagere, kamaliza ligi bila Majeraha!

Sambaza....

Kuna vingi vya kujifunza kutoka kwa Meddie Kagere. Wakati anasajiliwa Simba mengi yalizungumzwa hasa hasa kuhusiana na umri wake.

Inawezekana umri wake ni mkubwa sana lakini wachezaji wetu wanatakiwa kukaa na kujifunza vingi kutoka kwa Meddie Kagere.

Pamoja na kwamba Meddie Kagere kuonekana na umri mkubwa lakini ndiye alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu, mchezaji ɓora wa Simba , mfungaji bora wa Ligi kuu na klabu yake ya Simba.

Amewazidi wengi ambao wanaonekana ni vijana na wenye umri mdogo tofauti na yeye. Pamoja na kusemwa ana umri mkubwa lakini amezidi kuwazidi vijana hawa wenye umri mdogo.

Hicho ni kitu cha kwanza cha kujifunza kutoka kwa Meddie Kagere. Kitu cha pili na kikubwa ambacho Meddie Kagere anatoa somo kwa vijana wetu ni nidhamu yake aliyo nayo.

Meddie Kagere ana nidhamu ndani na nje ya uwanja. Ndani ya uwanja ana timiza majukumu yake vizuri ndiyo maana amefanikiwa kuwa mfuɓgaji ɓora na mchezaji bora wa ligi kuu.

Anajituma sana ndani ya uwanja na anafanya mazoezi sana ili kuhakikisha kiwango chake kinazidi kuimarika kila uchwao, kwa kifupi nidhamu ya mazoezi imemsaidia kufanya vizuri kwenye ligi.

Kagere kwenye moja ya mechi

Nidhamu nje ya uwanja imekuwa silaha kubwa kwake yeye kufanya vizuri ndani ya uwanja. Meddie Kagere anajitunza vizuri nje ya uwanja.

Hafanyi vitendo ambavyo vinahatarisha kiwango chake kushuka. Anajua kula vizuri na anakula kwa wakati sahihi, anajua muda upi sahihi wa kupumzika.

Ndiyo maana mpaka ligi inamalizika Meddie Kagere hajapata majeraha pamoja na kuonekana ni mchezaji ambaye ni mzee.

Na hii ni kwa sababu anajitunza vizuri sana , anakula vizuri, anapumzika vizuri hafanyi starehe ambazo zinahatarisha afya yake. Meddie Kagere ni somo ambalo wachezaji wetu wanatakiwa kulichukua na kulisoma vizuri.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.