Iddi Pazzi (2019)
Blog

Pazi : Mimi ndie Tanzania one

Sambaza....

Jina la Tanzania one limekua likitumika kwa walinda mlango mahiri wanaotokea nchini Tanzania katika nyakati tofauti kutokana na viwango vyao bora wawapo golini.

Toka enzi za kina Mwameja, Kaseja na leo hii Aishi Manula  tumekua tukiwaita “Tanzania One” lakini kumbe kuna mwenye jina lake ambae ndie alieanza kuitwa “Tanzania one” na mashabiki wa mpira Tanzania.

Idd Pazi kipa wa zamani wa Simba anasema yeye ndie mlinda mlango wakwanza kabisa kuitwa “Tanzania one”  halafu ndio walafuata kina Mwameja na wengine. Aliyasema hayo alipokua akiongea na wachezaji wa sasa wa Stars kuelekea mchezo dhidi ya Uganda katika mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa.

Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa Stars wakiongea na wachezaji wa sasa wa Stars.

Idd Pazi “Kama nilivyowaambia mimi ndie kipa wa kwanza kuitwa Tanzania one hata hawa wakina Mwameja wallitwa hilo jina baada yangu mimi. Enzi zangu nilikua hatari sana, hata wakati tunaenda Nigeria kwenye Afcon mwaka 1980 nilikua kipa namba tatu lakini tayari nilishajipambanua kua kipa hatari.”

Idd Pazi pia ndie kipa wakwanza wa Tanzania kucheza nje ya nchi kwa nafasi ya mlinda mlango.

“Mwaka 1997 nilipata dili kwa Mkaburu na sikuliacha nikaenda zangu Africa Kusini na kuandika historia ya kua kipa wa kwanza nchini kudaka nje ya mipaka ya Tanzania. Baada ya hapo pia nikaenda Indonesia na kukaa kwa misimu sita.”

Idd Pazi pia ni moja ya makipa waliokaa langoni kwa muda mrefu akicheza tangu mwaka 1977 mpaka alipostaafu mwaka 2002.

Kipa huyo ni moja ya mashujaa walioipeleka Tanzania katika Afcon ya mwaka 1980 alicheza pia katika klabu ya Simba Sports Club  na kuondoka mwaka 1993.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.