Blog

Picha hii inanibarikia sana hasa tunapokuja kwenye maana ya soka

Sambaza....

Nafahamu siku zote picha moja ina tafsiri rasmi na zisizo rasmi 1000 kutokana na mapokezi yako

Katika picha hii ni Makocha wawili wa @simbasctanzania kwa wakati huu Juma Mgunda na Seleman Malola.

Kwenye tafsiri yangu ya kwanza ni kuonesha ushirikiano wa hawa watu wawili kwenye benchi la ufundi

Hali hii inaonesha umoja uliopo na ushindi wa kimbinu na ufundi walio U- Implement kwenye timu kwa lugha nyepesi tunaweza kusema ni kujipogeza baada ya kufanikiwa jambo

Kwa matter ya seniority hapo Mgunda ni mkubwa kungine kwa hali zote umri na taaluma ya mchezo husika

Matola ni mdogo wa Mgunda kwa hali zote umri na kitaaluma pia ( mambo yetu ya level za CAF)

Japo ana silaha muhimu zaidi ya kuwa Mwenyeji sana ndani ya timu maana yake
Senior Mgunda anahaja pia ya kujifunza vitu vingi kwa mdogo wake huyu ambaye ndiyo mwenyeji wake kwa sasa

Mwisho kutoka kwangu ni kufurahi kuona sisi Makocha Wazawa tunarejea tena kuaminika kwa hizi timu kubwa

Haijalishi nini kitafuata kwa Mgunda lakini hadi hapa ni mshindi na ameonesha kitu kikubwa ikiwemo ikiwemo kuandika historia yake binafsi


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.