Ligi Kuu

Rasmi: Himid Mkami aachana na Azam

Sambaza....

Klabu ya soka ya Azam ya jijini Dar es Salaam imethibitisha kuachana na kiungo Himid Mao Mkami ambaye amekulia katika klabu hiyo baada ya kudumu kwa takribani miaka 10 tangu akiwa timu za vijana.

Taarifa za kuachana na Himid Mao, zimetolewa na afisa habari wa klabu hiyo Japhary Idd Maganga ambaye amesema wanamshukuru kwa namna ambavyo ameweza kuwasaidia kufikia mafanikio machache katika kipindi chote akiwa na timu hiyo.

Maganga amesema wanamtakia kila kheri katika maisha yake mapya ya soka ambapo amethibitisha kuwa Himid amewaomba kuondoka klabuni hapo ili kutafuta timu nje ya Tanzania kwenye changamoto zaidi.

Kwa muda mrefu tupo naye kwenye timu tangu akiwa na miaka 15, yeye ametuomba kuwa ana mipango yake ya kwenda kucheza soka nje ya nchi, na sisi kama klabu tumeona tumpe heshima kwa maana ni mchezaji ambaye amekuwa kwenye timu muda mrefu, na tunamshukuru kwa mchango wake alioutoa kwenye timu,” Maganga amesema.

Rekodi zinaonesha kuwa Himid Mao ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba na Timu ya Tanzania alijiunga na Azam Novemba 9, 2009 na mkataba wake unaonesha kuwa unaisha mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x