Robertinho
Stori

Robertinho: Nimeandaa Timu Kuifunga Yanga Mabao Mengi.

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la FA itakayofanyika katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga kocha wa Simba amesema ameiandaa timu yake vyema.

Yanga na Simba wanakwenda kukutana katika mchezo huo baada ya Simba kumfunga Singada FG Fc kwa mikwaku ya penati na Yanga wao waliwafunga Azam Fc mabao mawili kwa bila.

 

Akiongea na Waandishi wa habari Robertinho alisema “Nimeiandaa timu yangu kucheza vizuri wakati hawana mpira, kucheza kwenye eneo la mpinzani, kushambulia kwa nguvu, kufunga magoli na kufurahia mchezo,” alisema na kuongeza;

“Badala ya kucheza kwa kuwaza (mpinzani), mwisho wa yote, ushindi ndilo lengo letu kuu katika mchezo huu,” alimalizia Roberto Oliviera.

Kiungo wa Yanga Khalid Aucho akimuacha Clatous Chama wa Simba mara ya mwisho walipokutana katika mchezo wa Ngao ya Hisani.

Endapo Yanga watapa ushindi katika mchezo wa kesho watakua wamefanikiwa kulitwaa taji hilo mara tatu mfululizo tena mbele ya Simba, hivyo Simba wana nafasi kubwa ya kuamua kuwekewa au kuzuoa historia hiyo ya Yanga.

 

Sambaza....