Ligi Kuu

Ruvu Shooting warudisha mdomo wa Haji Manara !

Sambaza kwa marafiki....

Baada ya Yanga kufungwa na Ruvu Shooting goli moja kwa bila katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom , msemaji wa Simba Haji Manara anaonekana kufurahia matokeo hayo.

Akizungumza na mtandao huu Haji Manara amedai kuwa Yanga wamefungwa goli mbili, moja refa kabeba mpira kwapani.

” Wamepigwa mbili , ndiyo taarifa niliyo nayo, wamefungwa mbili bila moja refa kachukua mpira akauweka kwapani”.

Alipoulizwa kuhusu mechi yao ya kesho dhidi ya JKT Tanzania amedai kuwa wamejiandaa vizuri kwa mechi ya kesho.

“Sisi tumejiandaa vyema, tunamshukuru Mungu na tumuombe uhai kesho Inshallah tutaanza ligi vizuri”.

Alipoulizwa kuhusu kipigo cha UD Songo amedai timu zote kubwa huwa zinafungwa.

” Timu zote kubwa duniani huwa zinafungwa, hakuna timu kubwa ambayo haijawahi kufungwa. Timu zote kubwa duniani huwa zinafungwa”.

Alipoulizwa kuhusu kuarisha mkutano wake na waandishi wa habari hapo jana amedai kuwa alikuwa hayupo Tanzania, alikuwa mjini Cairo nchini Misri.

“Nimefika Tanzania saa kumi na robo, nilikuwa Cairo ndiyo maana mkutano wangu na waandishi wa habari hapo jana uliarishwa”. Alimalizia Haji Manara.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.