Saa 48 pekee, Thierry Henry kutimuliwa jumla jumla Monaco.

Sambaza....

Ukisikia “Breaking News” usishangae maana kwa sasa kama ni maji basi yatakuwa yameshafika shingoni.

Kocha wa Monaco na mchezaji wa zamani wa Arsenal na Barcelona, Thierry Henry yuko mbioni kufungashwa vilago jumla jumla baada ya kusimamishwa kwa muda katika klabu hiyo kutokana na matokeo mabaya ya timu katika msimamo wa kuu nchini Ufaransa.

Tangu achukue nafasi ya kuhudumu kama kocha mkuu, oktoba mwaka  jana, Monaco imefungwa mechi 12,  kati ya 21,  ikishinda mechi 3, na kutoa sare mechi 6, hii ni sawa na asilimia 20 ya ushindi kwa mechi zote.

Katika mechi hizo 21, Monaco imefunga magoli 19 na kufungwa magoli 36 ikishika nafasi  ya 19 kati ya 20  katika msimamo wa French Ligue I, ikiwa ni nafasi ya katikati miongoni mwa timu zinazopambana kutoshuka daraja.

Ikiwa na alama  15, inatofautiana na anayeshika mkia, timu ya Guingamp iliyopigwa 9 na PSG kwa alama 1 kwani Guingamp ina alama 14 pekee.  PSG ndio wanaoongoza ligi wakiwa na alama 53 nyuma ya alama  38 na Monaco ya Henry.

Tetesi zinadai kuwa, mabosi wa Monaco huenda wakafanya maamuzi magumu ya kumtimua kocha huyo ndani ya saa 48, na klabu hiyo kuchukuliwa na kocha wa awali Leonardo Jardim.

Tetesi za kutimuliwa kwake zimesambaa zaidi kufuatia kipigo cha goli 3-1 kutoka kwa Metz wanaoshiriki daraja la pili ( lige 2)  siku ya jumanne  katika kombe la “French Cup” ambao walionekana kama ” underdog” mbele ya Monaco katika uwanja wa Stade Louis II.

Akiwa kama kocha, Henry  amejaribu kupunguza kikosi chake, na kuhakikisha anabaki wa wambanaji lakini mambo kwake ndio yanazidi kumuendea mrama.

“tumepunguza kikosi, kwa namna moja ama nyingine lengo ni kusalia na wachezaji wenye malengo ya dhati natimu na wala sio malengo ya binafsi kwa siku za mbeleni, sasa tuko vitani” aliongea Henry katika mkutano na waandishi wa habari.

Mabosi wa Monaco tayari wameshamsimamisha Henry kwa muda usiojulikana kwa kile wanachodai ni kufikiria zaidi kuhusu uwepo wake katika timu ukilinganisha na matokeo ya Monaco kwa ujumla.

Kama lilivyo soka, kusikika kwa tetesi kama hizi ujue kabisa, muda si mrefu, mambo yatakuwa kama tunavyosikia. Taarifa zote utazipata hapa hapa  kandanda.co.tz.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x