Ligi Kuu

Sababu tatu kwanini Mbao wangeweza ifunga Simba

Sambaza....


Leo ligi kuu ya Tanzania inaendelea. Mchezo ambao unatazamwa sana kwa kiasi kikubwa Leo hii ni kati ya Simba na Mbao FC.

Simba atakuwa mwenyeji wa mchezo huu ambapo utapigwa kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro, uwanja ambao Simba wamechagua kama uwanja wa nyumbani kupisha marekebisho ya uwanja wa Taifa kwa ajili ya Afcon.

Sababu kwanini Mbao Fc ana nafasi kubwa ya kushinda hii mechi dhidi ya Simba.

KUTOKUWEPO KWA MANULA, OKWI NA CHAMA.

Leo Simba wanaingia kwenye mchezo huu bila kuwa na wachezaji wake ambao ni nyota msimu huu. Simba itawakosa Aishi Manula, Chama na Emmanuel Okwi.

Aishi Manula amekuwa mhimili mkubwa ndani ya safu ya ulinzi ya Simba, ambapo mpaka sasa hivi ana cleansheets 16 katika michezo 22 aliyocheza. Hivo kukosekana kwake kutakuwa pengo kubwa sana kwa Simba, pengo ambalo kama Mbao FC watalitumia vizuri wanaweza kuipa ushindi.

Emmanuel Okwi pia atakosekana huyu mpaka sasa hivi kwenye ligi kuu ya Tanzania bara amefanikiwa kufunga magoli saba (7).

Huku Chama akiwa amefanikiwa kufunga magoli manne (4) mpaka sasa hivi kwenye ligi kuu Tanzania bara huku akiwa ni mtengenezaji mabao.

Kwa hiyo Simba wanamkosa Mlinzi mahiri (Aishi Manula, wanamkosa mfungaji mahiri wa magoli Emmanuel Okwi na mtengenezaji wa magoli na mfungaji wa magoli Chama.

UWANJA WA JAMHURI

Kuna faida kubwa sana kwa Mbao kucheza na Simba katika uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa sababu aina ya eneo la kuchezea.

Aina la eneo la kuchezea katika uwanja wa Jamhuri linafanana kabisa na eneo la kuchezea la uwanja wa CCM Kirumba.

Aina hii ya eneo la kuchezea ni rafiki kwa Mbao FC kwa sababu wamezoea kucheza kwenye aina hii ya uwanja. Wakati Simba wamezoea kucheza kwenye aina ya eneo la kuchezea ambalo halifananii na kiwanja cha Jamhuri Morogoro.

PENZI JIPYA LA SALUM MAYANGA

Ndiye kocha mpya wa Mbao FC kwa sasa. Bila shaka atanufaika na penzi jipya kwa sababu kuna kawaida wachezaji wengi huwa wanataka kumuonesha kocha mpya uwezo wao ili kumshawishi.

Hivo kwenye mechi hii wachezaji wa Mbao FC watajituma sana ili kumshawishi Kocha Salum Mayanga. Faida nyingine ambayo Salum Mayanga ni kuwa atakuwa kwao kwenye uwanja wake wa nyumbani kwao.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.