Kagere kwenye moja ya mechi
Ligi Kuu

Sababu tatu kwanini Singida United wataifunga Simba

Sambaza....

Leo Singida United watawakaribisha Simba katika uwanja wao wa nyumbani wa Namfua. Simba inahitaji sare tu katika mchezo huu ili kuwa mabingwa.

Kiufundi, mechi hii itakuwa ngumu sana kwa Simba na kuna asilimia kubwa leo Simba wasitangaze ubingwa kwenye ardhi ya Singida. Hizi ni sababu tatu kwanini Singida United watazuia sherehe za Simba.

1: MATOKEO YA SINGIDA UNITED KATIKA UWANJA WAKE WA NYUMBANI.

Hivi karibuni Singida United wamekuwa na matokeo mazuri sana katika uwanja wake wa nyumbani wa Namfua.

Katika mechi tano zilizopita wameshinda mechi tatu ( 3 ) na kutoka sare michezo miwili (2). Huku wakiwa wamefunga goli kwenye mechi nne.

Ni mechi moja tu ambayo hawakufanikiwa kufunga goli. Wakiwa wamefunga magoli nane (8) katika mechi tano (5) zilizopita katika uwanja wake wa nyumbani, huku wakiwa wamefungwa magoli manne (4).

2: UWANJA WA NYUMBANI

Pamoja na kwamba hivi karibuni wamekuwa na matokeo mazuri kwenye uwanja wao wa nyumbani, pia leo hii watakuwa na mashabiki wao.

Watakuwa na mtaji wa mashabiki ambao watakuwa wanawaunga mkono ili wabaki kwenye ligi kuu ya Tanzania. Hivo nguvu watakayopata Singida United kutoka kwa mashabiki wanaweza kufanya vizuri kwenye mechi hii.

3: PRESHA YA KUSHUKA DARAJA.

Singida United wako na alama arobaini tano (45) . Wako katika hati hati ya kushuka daraja, mtu ambaye anaweza kumfikia Sindiga United ana alama arobaini mbili (42) ambaye yupo kwenye hati hati ya kushuka daraja, kwa hiyo Singida United watawekeza nguvu kwenye mechi hii ili kupata alama ambazo zitawafanya wao waondokane kushuka daraja.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.