Ligi

Sibomana azidi kumburuza Kagere

Sambaza....

Ule mchezo ambao ulitakiwa kuchezwa katika uwanja Sokoine mjini Mbeya Kati ya Prisons na Yanga na kuhamishwa kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa kutokana na uwanja wa Sokoine kuharibiwa vibaya eneo la kuchezea.

Mechi hiyo ambayo imechezwa muda wa saa kumi jioni ya Leo tumeshuhudia Yanga akiibuka na ushindi wa goli moja kwa bila. Goli ambalo limefungwa na Patrick Sibomana.

Patrick Sibomana tangu mwezi Novemba amefanikiwa kufunga magoli manne na kutoa Pasi moja ya goli. Mchezaji pekee ambaye anamshinda Patrick Sibomana katika ufungaji wa magoli tangu November mpaka sasa hivi ni Zaureshi Saliboko aliyegunga magoli 5.

Kwa maana hiyo Baada ya kufunga goli Leo anazidi kumkimbiza Meddie Kagere ambaye kwa mwezi November mpaka mwezi wa kumi na mbili amezidiwa idadi ya magoli na Patrick Sibomana.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.