Mfungaji Bora mwezi wa Tisa wa ligi Kuu Tanzania bara, Eliud Ambokile, akiwa na zawadi yake kutoka katika tovuti ya kandanda ya kumpongeza.
Uhamisho

Siji Yanga, nitabaki TP Mazembe-Ambokile

Mshambuliaji wa zamani wa Mbaya City ambaye kwa sasa yuko TP Mazembe amesema bado anaendelea kupigana ili aweze kupata namba kwenye kikosi cha TP Mazembe

Sambaza....

 

Mshambuliaji wa Tanzania Eliud Ambokile ambaye kwa sasa yuko katika klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo amedai kuwa kwa sasa hafikirii kuondoka TP Mazembe kwa sasa ndiyo sehemu sahihi kwa afya ya mpira wake kwa sasa .

“Sifikirii kuondoka TP Mazembe kwa sasa kutokana na hali ya mazingira ya klabu hii , mazingira ya TP Mazembe ni mazingira ambayo yananipa nafasi kubwa ya Mimi kujikuza kwenye kipaji changu na kipaji changu kuwa na maendeleo”- alisema Eliud Ambokile wakati anazungumza na Wasafi Fm.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mbeya City ameongeza kuwa kwa sasa kupata namba kwenye kikosi cha TP Mazembe ni ngumu kwa sababu na aina ya kikosi alichokutana nacho ila yuko kwenye mapambano ya kupigania kupata namba kwenye kikosi cha TP Mazembe.

Ambokile

“Wakati nakuja TP Mazembe nilikuta tayari kikosi kimeundwa vizuri na mwalimu alikuwa na kikosi chake na kikosi kilikuwa na wachezaji imara na bora kwa hiyo ilikuwa mtihani mkubwa kupambana mpaka kupata nafasi kwenye kikosi cha TP Mazembe , ila kwa sasa napigana kwa kiasi kikubwa kupata namba kwenye kikosi cha TP Mazembe”-alimalizia mchezaji huyo nyota wa Tanzania ambaye awali Kulikuwa na tetesi ya yeye kwenda Yanga , kusema kwake kuendelea kuwepo TP Mazembe kunafanya kuua tetesi za yeye kwenda Yanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.