Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba wapo katika mipango ya kutafuta kambi ya muda mfupi kuelekea mchezo wao wa Ligi ya mabingwa Afrika na tayari Jiji la Nairobi linapigiwa upatu.

Simba watavaana na Power Dynamos September 16 mwaka huu katika dimba la Levy Mwanawasa Ndola Zambia katika mchezo wakwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Afrika.

 

Kufuatia mapumziko ya kuzipisha mechi za timu za Taifa Simba wameamua kutimkia nchini Nairobi ambapo wataweka kambi huko ambapo hali ya hewa inafana na ile ya Ndola Zambia.

Chanzo kutoka Kenya kinataarifu juu ya kambi hiyo ambayo itakua sio chini ya siku tano na Simba watapata nafasi ya kukipiga na Gor Mahia japo rasmi uongozi wa Simba bado hawajathibitisha hilo.

Wachezaji wa Simba wakiwa mazoezini.

Wekundu wa Msimbazi wamepania kufanya vyema katika ligi ya mabingwa na wameona ni wakati sahihi kwa wao kuendelea na mazoezi chini ya kocha mkuu Robert Oliveira ambae bado hajakisuka kikosi hicho kwa asiilimia zote.

Tayari msemaji wa Simba Ahmed Ally wiki alisema wanatafuta sehemu ambayo wataweka kambi fupi kujindaa na mchezo huo ambao umeshika hatma ya Simba yakushiriki hatua ya makundi msimu huu.

Sambaza....