Stori

Simba ni Kikubwa na Historia Zaidi.

Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba kesho watafikia tamati ya wiki ya Simba kwa kucheza mchezo wa kirafiki wakimataifa dhidi ya Power Dynamos kutoka Zambia.

Wageni hao kutoka Zambia ndio watakaohitimisha tamasha la Simba day ambapo watacheza na Simba katika mchezo ambao itawapa fursa mashabiki wa Simba kuiona timu yao kwa mara ya kwanza msimu huu.

Kuelekea mchezo huo ambapo washabiki wengi wa Simba wana hamu ya kuwaona nyota wao wapya kocha mkuu wa timu hiyo Robertinho Oliveira ameshatema cheche.

Kuelekea mchezo huo Mbrazil huyo amesema “Kesho ni siku muhimu kwa Wanasimba wote, wanataka kuja kuiona timu yao. Na niwahakikishie tuna tima imara msimu huu,” alisema na kuongeza

“Tuna mashindano mengi msimu huu, mchezo dhidi ya Power Dynamos utakuwa kipimo kizuri kwetu.”

Che Fonde Malone.

Nae mchezaji mpya wa timu hiyo ambae amebeba matumaini makubwa ya mashabiki wa Simba Che Fonde Malone kutoka Cameroon amesema kwake kesho ni siku kubwa huku akiwa na hamu ya mashabiki uwanjani.

“Kesho ni siku kubwa, tunajua mashabiki wana hamu ya kuiona timu yao. Wanataka waone timu inachezaje pamoja na wachezaji wapya, nafurahi kuwa sehemu ya kikosi.”

“Binafsi sina hofu ya wingi wa mashabiki watakaojitokeza kwa wingi uwanjani kesho, nimejipanga kuhakikisha ninafanya vizuri kama nitapata nafasi ya kucheza,” alisema Malone

Sambaza....