Michezo mitano ilipigwa jana katika viwanja mbalimbali nchini katika muendelezo wa Ligi Kuu Bara huku mshambuliaji wa Biashara United akiingia katika vitabu vya rekodi msimu huu.
Timu ya Tanzania jana ilikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri, katika mchezo huo Tanzania ilipoteza kwa kufungwa bao moja bila. Je Kiwango cha timu umekikubali? Pitia uchambuzi huu
Klabu ya Simba SC iliwatunikia wachezaji wake tuzo mbalimbali usiku uliopita ikiwa ni muendelezo wa tuzo hizo zilizoanza kutolewa msimu uliopita chini ya mwekezaji mkuu wa klabu hiyo-tajiri, Mohamed Dewji ‘MO’.
Baada ya Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kufunga mabao matatu katika mechi moja kwa mara ya kwanza msimu huu katika mchezo dhidi ya Coastal Union ni wazi sasa katika vita ya ufungaji bora imetawaliwa na wachezaji kutoka Simba sc
Tovuti ya kandanda imekuandalia takwimu za kila mchezaji kuangalia timu anayotoka ipo katika nafasi ya ngapi kati ya timu ngapi, alama timu ilizonazo katika ligi husika. Adi Yusuph na John Bocco vinara katika timu zao.