Ligi Kuu

Simba Siyo mabingwa sahihi-Zahera

Sambaza....

Kocha mkuu wa Yanga amegoma kuwapongeza Simba kama mabingwa kwa sababu hawakustahili huu ubingwa.

Kocha huyo kutoka DRC Congo, amedai kuwa Simba hawakustahili huu ubingwa na haoni sababu ya yeye kuwapongeza ubingwa.

“Simba hawajachukua ubingwa , Simba wamepewa ubingwa”.

“Ubingwa huchukuliwa kwa nguvu na siyo kwa kupewa kama ambavyo wamepewa Simba”.

“Na walianza kupewa ubingwa kwenye raundi ya pili baada ya sisi kuonekana tunauwezo kuchukua ubingwa”.

“Mimi siwezi kuwapa hongera kwa sababu hawakustahili ubingwa, kwenye watu saba wawili tu ndiyo watakubali ubingwa wa Simba”.

“Hata wachezaji wa Simba ukiwauliza watakuambia kabisa hawakustahili ubingwa huu”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.