Mabingwa Afrika

Simba: Tumefufuka kwelikweli, CAF ndio wapanga ratiba

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imetema cheche kuelekea mchezo wake unaofwata wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kutanganza vita kwa Waganda hao.

Kupitia msemaji wake Ahmed Ally Simba wamesema watacheza mchezo wao dhidi ya Vipers saa moja jioni na kujitoa lawama ya muda wa mechi wakisema CAF ndio wanaopanga ratiba.

“Mechi dhidi ya Vipers itakuwa Jumanne Machi 7, 2023 saa 1:00 usiku. Ratiba inapangwa na CAF na kati ya hizo mechi kuna mchezo unapangwa kuchezwa katikati ya wiki. Sisi tunatii maagizo ya CAF, na sio Simba peke yake bali timu zote zinazochesha mashindano ya CAF.”

Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba Sc

Ahmed Ally pia amesema tayari kikosi kimeingia kambini kujiandaa na mchezo huo muhimu ambao utaamua hatma yao yakufuzu hatua ya robo fainali.

Ahmed Ally “Kikosi kimeingia kambini leo baada ya mchezo wa jana wa ASFC, na leo jioni kikosi kitaanza mazoezi. Bado siku tano kabla ya mchezo dhidi ya Vipers, tumeingia kambini kwa umuhimu wa mchezo wenyewe, tunauhitaji kwelikweli.”

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao pekee la Henock Inonga dhidi ya Vipers.

“Tulikwenda kufufukia Uganda, na kweli tumefufuka. Jumanne ni mechi ya marudio katika mechi hii tunakwenda kuamua hatma ya Simba kwenye michuano ya CAF. Tukimpiga tutafikisha alama 6 na kuanza kuchungulia robo fainali

“Hatupo tayari kuishia hatua ya makundi. Tulikwenda kuchukua alama tatu kwa Vipers lakini hatujamaliza, tunakwenda kuzichukua alama zingine hapa nyumbani. Niseme tu tuko tayari kwa mchezo.” Ahmed Ally alimalizia

Sambaza....