Mabingwa Afrika

Simba Wamefeli Hawastahili Pongezi Zozote.

Sambaza....

Ilitoka wapi dhana ya kufa kiume? Nani alileta huu msemo na alikua na maana gani?. Simba jana imetolewa tena katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama ambavyo wamekua wakitolewa siku zote lakini sijui kwanini mashabaki wanaamini Simba inapaswa kupongezwa!?

Simba ilitolewa na Wydad Casablanca kwa mikwaju ya matuta baada ya mchezo kumalizika kwa kufungwa bao moja bila na hivyo kufanya kuwa sare ya bao moja kwa moja kwa ya jumla baada ya wao kupata ushindi kama huo walipokua nyumbani.

Hakuna jinsi yoyote ambayo Simba watapaswa wajipongeze ama wajisifie kutokana na matokeo hayo kwasababu bado hawajafikia lengo lao lakwenda nusu fainali kama ambavyo walishasema tangu mwanzoni mwa msimu.

Mshambuliaji wa Simba Kibu Denis akimuacha mlinzi wa Wydad Casablanca

Lengo kuu la Simba lilikua ni kucheza nusu fainali baada ya kucheza robo fainali tatu miaka ya hivi karibuni na si kutolewa kwa tabu katika robo fainali. Hivyo licha ya kucheza vyema  katika uwanja mgumu wa Mohamed wa tano dhidi ya bingwa mtetezi bado hawana chakujivunia.

Msimu uliomalizika Simba walipata matokeo kama haya katika kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates kwa kutolewa kwa matuta lakini kaunzia pale walipaswa wajifunze kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani lakini pia walishapata joto ya jiwe jinsi ambavyo mikwaju ya matuta inapaswa ipigwe. 

Pengine mashabiki wa Simba walijua wanaingia katika uwanja mgumu dhidi ya mpinzani mgumu na kutegemea huenda timu yao ingefungwa mabao mengi na kupoteza kirahisi lakini haikua hivyo kutokana na mpango mzuri wa mechi alioingia nao Babu Robertinho na hivyo kuona wamepiga hatua lakini ukweli unabaki palepale Simba imefeli tena kwa mara nyingine kuvuka na kwenda nusu fainali.

Wachezaji wa Simba baada ya mchezo kumalizika

Ni kweli Simba walicheza vyema kwa kufanikiwa kuzuia hatari zote za Wydad na kupelekea kufungwa bao moja pekee kwa makosa ya Joash Onyango na Ally Salim lakini walipaswa angalau kulisogelea lango la Wydad walau kujaribu bahati yao maana timu inayotaka kwenda nusu fainali haiwezi kucheza dakika 90 bila kupiga shuti lililolenga lango.

Simba wakubali ukweli kwamba wametolewa na hawajafikia lengo lao na si kutumia kivuli chakusema wamejitahidi ama wamekufa kiume.

Simba sasa wanapaswa kuendelea walipoishia kwakuongeza umakini ziadi katika kusajili wachezaji wazuri zaidi, kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kuendelea kucheza vyema katika viwanja vya ugenini. 

 

Sambaza....