Stori

Simba Wanavyotoka Uwanjani na Kuingia Mtaani Kabisa

Sambaza....

Simba wameitoa timu yao kiwanjani, ofisini na wameipeleka chini kabisa mashuleni kwa watoto. Sijui kama wengi tumewalewa Simba SC na mpango wao huu.

Kwangu ndani ya mpango huu kuna faida mbili ndani yake. Nitakuelezea faida zenyewe. Mosi, Simba SC wanawatengeneza mashabiki wao wa kesho katika njia laini kabisa.

 

Shabiki wa mpira anaandaliwa. Anawekewa mazingira ya kukipenda kitu. Hiki wanachokifanya Simba SC ndiyo maandalizi yenyewe ya kuwa na shabiki mfia timu wa kesho. Vizuri Mnyama .

Pili, kama kuna mchezaji ambaye anaweza kupatikana katika kundi hili basi itakuwa jambo jema. Ndani ya hii inakuwa umempata mchezaji na umempata shabiki.

Kwangu Simba SC wametumia akili kubwa kuja na mpango huu. Timu nyingi kubwa zilizofanikiwa zilianza na harakati za namna hii.

Imani Kajula Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba.

Nadhani ni wakati wa timu nyingine nazo kuja na vitu vya namna hii ili kuandaa mashabiki wao. Vizuri huwa vinaigwa.

Jana kupitia Mtendaji wake mkuu wa klabu ya Simba Imani Kajula alitambulisha mpango mpya wa klabu yao unaojulikana kama “Back to school”  akiwa sambamba na mkuu wa program za vijana Patrick Rweyemamu, mwakilishi kutoka NMB Hassan Bumbuli na baadhi ya watoto waliowawakilisha wenzao.

Kupitia mpango huo watoto watanufaika na kupata nafasi ya kuhudhuria mechi za Simba, kupata bidhaa za klabu pamoja na kuendeleza vipaji vyao kupitia ushirikiano wa shule zao na Simba.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x