Simba Sc
Mabingwa Afrika

Simba Yaanza Safari ya Morocco Mapema.

Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba tayari wameanza safari ya kuelekea nchini Morocco kucheza mchezo wao wa pili wa marudiano wa robo fainali dhdi ya wenyeji wao Wydad Casablanca. 

Simba wanakwenda nchini Morocco wakiwa na uongozi wa bao moja bila walioupata katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa. Goli la Simba lilifungwa na Jean Baleke katika kipindi cha kwanza.

Meneja wa Habari na Mawalisiano wa klabu Ahmed Ally amesema “Kikosi cha Simba kinaondoka leo usiku kuelekea Morocco tayari kwa mchezo wa maruadiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Ijumaa.”

Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba Sc

Katika safari hiyo Simba haitakwenda wote kwa pamoja kutokana na changamoto za usafiri wa ndege na hivyo watasafiri kwa mafungu mawili.

Ahmed Ally “Msafara utagawanyika makundi mawili, Kundi la kwanza litaondoka leo na litakuwa watu na 29 wachezaji na benchi la ufundi wakati la pili litaondoka kesho likiwa na watu 20.”

Simba wanakwenda nchini humo wakiwa na mtaji wa bao moja huku wakihitaji sare pekee ili kuvuka kwenda nusu fainali ama wakifungwa iwe tofauti ya bao pekee na hivyo bao la ugenini litawavusha.

Kibu Denis na Jean Baleke wakishangilia bao pekee la Simba katika mchezo wa kwanza wa robo fainali.

Licha ya kupata ushindi mwembamba nyumbani lakini tayari Simba wameshasema watarudia ya miaka 20 nyuma walipowatoa Zamalek ya Misri ambao walikua mabingwa watetezi kama ambavyo sasa Wydad ni mabingwa watetezi.

Simba watahitaji kucheza mechi ya machozi, jasho na damu kupambana katika mchezo huo ili kuishi ndoto zao lakini pia wanapaswa kujiandaa na kukabiliana na mashabiki wa Wydad ambao wakiwa kwao huwa wanashangilia mwanzo mpaka mwisho wa mchezo. 

Sambaza....