Willy Esomba Onana akishangilia bao katika mchezo wa Simba Day dhidi ya Power Dynamos
Stori

Simba Yafanya Shoo ya Kibabe Mbele ya Mashabiki Wake Lukuki.

Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kumaliza siku yao kibabe kwa kuibuka na ushidi wa mabao mawili kwa sifuri mbele ya Power Dynamos katika mchezo ulioshuhudiwa na Rais wa nchi Daktari Samia Suluhu Hassan.

Katika mchezo huo uliopigwa jioni katika Dimba la Benjamin Mkapa kuhitimisha shughuli nyingine za burudani pamoja na michezo mingine ya kirafiki iliyotangua kiwanjani hapo.

Usajili wa Simba umeonekana kulipa mapema kwani magoli hayo mawili yaliyowapa ushindi yalifungwa na nyota wapya waliojiunga nao hivi karibuni katika usajili huu.

Ni Willy Onana katika dakika ya tano na Fabrice Ngoma katika dakika ya 75 ndio waliofanikiwa kuipa ushindi Simba, kwa maana wakifunga bao kila kipindi katika mchezo huo.

Fabrice Ngoma.

Ama kwa hakika mashabiki wa Lunyasi waliojitokeza kwa wingi wamewaona wachezaji wao wapya waliokua na kiu ya kuwatazama baada ya kusajiliwa na klabu yao.

Sasa kwa Simba kituo kinachofuata ni mkoani Tanga katika michezo ya Ngao ya Jamii ambapo watacheza mchezo wao wakwanza August 10 dhidi ya Singida Fountaine Gate Fc katika dimba la Mkwakwani.

Sambaza....