Sambaza....

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ”Taifa Stars” tayari kipo kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu katika fainali za mataifa ya Africa (AFCON) zitakazofanyika nchini Cameroon mwaka 2019. Taifa stars inajiandaa na mchezo wake wa pili wa kufuzu dhidi ya Uganda utakaopigwa jijini Kampala katika dimba la Nambolee.

Samata na Ulimwengu

Tayari kikosi hicho kimeshaingia kambini chini ya mwalimu Emmanuel Eminike, huku kikifanya mazoezi katika uwanja wa Bokko Beach Veterans na Uwanja wa Taifa Dar es salaam. Achana na wachezaji wanaocheza ligi ya ndani waliowahi kufika kambini kama ambavyo mwalimu alivyopendekeza, swala ni kuongezeka kwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ya Tanzania.

Inawezekana ikawa ni kwa mara ya kwanza kikosi cha Taifa Stars kikawa kinajumuisha wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi huku idadi yao ikifikia wachezaji 9. Walinzi wawili, viungo watatu na washambuliaji wanne wanatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho huku wengi wao wakiwa wameshaanza kuwasili.

Msuva akiwa njiani kujiunga na Stars

Rashid Mandawa (BDF XI -Botswana), Hassan Kessy (Nkana Red devils- Zambia), Abdi Banda (Baroka- Africa Kusini), Thomas Ulimwengu ”Buffalo” (Al Hilal- Sudan) na Simon Msuva (Difaa el Jadida) ,wote hawa wakitokea bara la Africa. Pamoja na Mbwana Sammata(KRC Genk- Belgium), Farid Mussa na Shabani Idd Chilunda (CD-Tenerife – Spain).

Kilio cha Watanzania wengi cha kua na timu ya Taifa yenye wachezaji wengi kinaelekea kuanza kupata majibu sasa. Hivyo tunaenda katika mchezo dhidi ya Uganda tukiwa na chachu ya wachezaji wengi wa nje huku tukiamini watatusaidia katika kufuzu Afcon 2019 Cameroon.

Sambaza....