Msemaji wa TFF Cliford Marion Ndimbo tayari ametaja viingilio vya mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya jioni siku ya Jumapili.
Zamani tulikuwa na kundi dogo la wachezaji wanaocheza nje. Hawakuwa wanafika hata watano, lakini hivi sasa tunaweza kuita wachezaji 17 wanaocheza nje bila kujumuisha wachezaji wa ndani.