
Wanachama wa Yanga
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kugombea Uongozi katika Klabu ya Young Africans, kwa mujibu wa taarifa toka TFF imesema.
Zoezi hilo limeongezwa siku 5 na sasa litakwenda mpaka Novemba 19,2018 ambapo awali zoezi lilikuwa linafikia tamati leo Novemba 14,2018.
Wanachama tayari wameanza kujitokeza katika zoezi hilo la uchukuaji na urudishaji wa fomu.
Aidha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Young Africans zinatarajia kukutana Ijumaa Novemba 16,2018
Uchaguzi wa Young Africans unatarajia kufanyika Januari 13,2019 nafasi zinazogombewa zikiwa ni Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na Wajumbe 4 wa Kamati ya Utendaji.
Unaweza soma hizi pia..
Alli Kamwe: Lengo Yanga na sio Mayele!
Mayele ni mchezaji muhimu kwenye Timu. Yanga inamuhitaji zaidi akiwa Fiti uwanjani kuliko yeye anavyokihitaji kiatu cha Ufungaji bora kabatini kwake.
Msemaji Simba: Mambo ni magumu!
Kila mwanasimba anatakiwa kufahamu hilo na kukubali mambo ni magumu.
Kola na mfupa uliomshinda Mayele!
Licha ya Fiston Mayele kusifiwa na kuoneoana ni moja ya washambuliaji hatari katika Ligi lakini hakufanikiwa kufunga
Mbinu mpya za Yanga zilizoacha lawama kwa kipa wa Dodoma Jiji
Nasredeen Nabi ilimlazimu kutoka katika mfumo wake wa siku zote wa kumtegemea Fiston Mayele na kubadili mbinu ili kupata ushindi.