
Ahmad Ahmad (Kulia) wakifuatilia mechi ya AFCON U17 viwanja vya Chamazi, Dar es Salaam.
- Alli Kamwe: Lengo Yanga na sio Mayele!
- Stars mpya ni Himid na Sure Boy!
- Msemaji Simba: Mambo ni magumu!
- Kola na mfupa uliomshinda Mayele!
- George Mpole anaishi ndoto zetu!
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwa Rais wa TFF kupewa fedha na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) zinazodaiwa ni fedha za rushwa, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kutoka katika ofisi ya TFF jioni hii.
Tuhuma hizo ambazo hapo kabla zilifafanukiwa katika tovuti ya kandanda, zimetiliwa mkazo zaidi na Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred ambaye pia amefafanua kwa kina tuhuma hizo.
Kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF iliyokutana Mei 8,2017 Bahrain kilipitisha maamuzi ya fedha mbalimbali uliokua na mchanganuo wa sehemu ya maendeleo na kiasi kingine kikielekezwa kwa Marais wa Mashirikisho Barani Afrika kuwasaidia katik mizunguko mbalimbali ya mpira wa miguu kwakuwa hawalipwi mshahara.
Maamuzi yaliyopitishwa ilikua ni kila Shirikisho kupatiwa 100,000 USD ambazo katika mgawanyo huo imeelekezwa Rais wa kila Shirikisho atapatiwa 20,000 USD,Maendeleo Soka la Vijana 50,000 USD na kiasi cha 30,000 USD kusaidia tahadhari kwa Waamuzi.

Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia baada ya mgawo huo kuingia aliuelekeza kutumika kwa shughuli mbalimbali za Shirikisho.
Hivyo basi shirikisho limekanusha taarifa zote zinazomuhusisha Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia kuchukua fedha hizo licha ya kuwa zimepitishwa katika vikao halali vya CAF.
TFF inawasiliana na Wanasheria wake ili wachukue hatua dhidi ya watu wanaosambaza taarifa hizi.
Unaweza soma hizi pia..
Waandishi wa habari za michezo waigalagaza Unitalent.
Unitalent hawakuishia tuu kufungwa mabao mawili lakini pia waliteseka uwanjani haswa katika eneo la kiungo
Kwanini Boban Hakuyapenda Maisha Ya Ulaya…?
Yumkini Haruna Moshi alishawishiwa kutokukipenda ambacho kingemsaidia maishani. Soma stori hii
Manara: Tunataka kuujaza uwanja Jumamosi!
Msemaji huyo pia ameonyesha ni kwa kiasi gani wamedhamiria kuujaza uwanja huku akitangaza neema kwa mashabiki wa Yanga wataokata tiketi kwenda uwanjani.
Hivi ndivyo tulivyomuua Samatta wetu.
Mimi siyo mpenzi wa mpira wa miguu ila nilisikia Rafiki zake wakimwiita Ronaldinho Gaucho,