Papy
Uhamisho

Tshishimbi kuondoka Yanga, arudisha pesa za GSM

Sambaza....

Kiungo mahiri wa klabu ya Yanga Papy Kabamba Tshishimbi ameshamaliza mkataba na Yanga , mpaka sasa hivi inavyoonekana hakuna mazungumzo ambayo yameshafanyika kati yake na Yanga kuhusu kuongeza mkataba. Papy Kabamba Tshishimbi alifanya mazungumzo na mtandao huu wa www.kandanda.co.tz , kwanza alisema msimu uliopita ulikuwa mbaya kwake.

“Nashukuru Mungu msimu umeisha salama. Msimu haukuwa mzuri kwangu na kwa timu kwa ujumla , hata mimi sijacheza mechi nyingi kwa sababu ya kuwa majeruhi.

“Kwangu mimi haukuwa msimu mzuri sana kwa sababu timu haijashinda kombe , hauwezi ukawa msimu mzuri wakati timu haijashinda kombe”. Alisema Papy Tshishimbi.

Papy Kabamba Tshishimbi.

Alipoulizwa ni vitu gani ambavyo vimesababisha Yanga isiwe na msimu mzuri , Papy Kabamba Tshishimbi alidai kuwa kuna vitu vingi ambavyo vimesababisha wawe na msimu mbaya ikiwemo wachezaji wenyewe.

“Kuna vitu vingi ambavyo vimesababisha tusiwe na msimu mzuri kwenye timu kwanza hata sisi wachezaji tumesababisha tusiwe na msimu mzuri”.

Alipoulizwa kuhusiana na kurudisha pesa za usajili wa Yanga , Tshishimbi alionekana kukwepa kuhusiana na suala hili na hakutaka kabisa kuongelea masuala ya usajili na klabu yake ya zamani ya Yanga.

“Kitu chochote kuhusiana na Yanga siwezi kukiongelea kwenye media kwa sababu Yanga ni familia , nimeitumikia kwa muda mrefu kwa hiyo siwezi kuongelea kwenye media labda uongozi uanze wenyewe kuongelea.

“Mpaka sasa hivi kulikuwa na makubaliano kati ya klabu na klabu ambayo yalikuwa haijakamilika. Natumaini mpaka kufika kesho tutakuwa tumekubaliana na Simba ni kiasi gani ambacho wanatakiwa kutupa” alimalizia Papy Kabamba Tshishimbi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.