Blog

Tulipiga ‘Sex football’ iliyokosa Kiguu cha kushoto!

Sambaza....

Katika mchezo wa marudiano baina ya Tanzania na Burundi, Hakika Taifa stars pamoja na yote ilipata ushindi wa mbinde kwa maana ya changamoto ya mikwaju ya penati. Ila kiuhalisia timu ilicheza mpira mkubwa, mwingi usiopimika katika mzani.

Wapwa katika mchezo wa mpira wa miguu kiu kubwa ya mashabiki ni kuona goli likifungwa. Lakini goli lina ladha yake kama kuna mipango andamizi nyuma yake kabla ya kupatikana (build up). Kwa kile nilichokiona katika mechi ya Stars vs Burundi ndicho nachelea kusema kulikuwa na ufundi mkubwa sana, umiliki mpira wa hali ya juu pasi au gonga maridhawa kwa mtiririko.

-Dilunga

Kikawaida timu za bongo ni ngumu kuona zinapiga pasi kuanzia 6 kwenda juu, hivyo kwa Taifa stars dhidi ya Burundi niliona pasi nyingi za kumwaga! Lakini pamoja na ladha na ufundi mkubwa wa kiwango hicho kwanini hatukupata ushindi wa moja kwa moja kwenye dk 90 hadi tukaenda 120 nazo zikashindwa kutupa ushindi?

Wapwa zangu binafsi nachelea kusema kukosekana kwa mguu wa kushoto halisi kwenye nafasi ya winga. Katika kikosi kilichoanza hakukukuwa na winga wa kushoto (natural left feeter) na mbaya zaidi timu ilikuwa inatokea kushoto muda mwingi. Beki wa upande wa kulia wa Intamba Murugamba alionekana kuwa uchochoro toka dakika ya kwanza hadi ya mwisho, timu ilipata nafasi za kutosha kutoka upande huu.

-Farid Musa

Wapwa, tatizo linaanzia wapi? Kila aliyepata nafasi kuwa na mipira eneo lile alishindwa kabisa kupiga kross yenye macho kuwapasia washambuliaji. Wote waliopita eneo lile walikutana na tatizo la kross (curve ) au top corner zenye tija kwa washambuliaji wa kati.  Kila aliyefungulia kule alikosa upigaji krossi wenye macho, hata alipo ingia bwana mdogo Farid Musa pamoja na kuwa ni natural left feeter (Orthodox) hakuwa upande ule na alijaribu kutimiza majukumu yake vyema. Lakini hakuna hata mpira moja alioupata akifunguliwa kushoto ili aweze kumimina kross!

-Samatta (Katikati)

Pamoja na ukweli miguu ya kushoto ni ni adimu sana duniani hasa kwenye nafasi ya winga wa kulia na ninaweza kusema ni janga la kidunia maana hata Uingereza hawakuwahi kupata winga wa kushoto tangu alivyoondoka Steve Mc Manaman. Hadi leo ni takribani miaka 20. Japo wenzetu wana academy ambazo wanaweza kumbadili au kumjenga mtu katika footwork nzuri kwa ya matumizi ya miguu yote miwili kwa usahihi, lakini kwetu tatizo hili lipo hata kwa mchezaji mkubwa wa Tanzania kwa maana ya Mbwana Samatta kushindwa kupiga kross za mguu wa kushoto,  kuna moja ya mchezaji alishindwa kupiga kross kwa mguu wa kushoto akalazimika kupiga outer kwa mguu wa kulia, sehemu ambayo alipaswa kucheep kidogo kwa kushoto!

Steve Mcmanaman

Wapwa kwa jicho langu la ufundi naweza sema tatizo la matumizi ya mguu wa kushoto ni janga kubwa sana ndani ya kikosi cha Taifa stars na unapaswa kufahamu ki-fizikia kuna nafasi mbili za kiuchezaji 3 na 11 zinataka mchezaji halisi mwenye kutumia mguu wa kushoto natural, otherwise benchi la ufundi likubali kumtumia Farid Musa kama winga wa kushoto.

My team my choice Alez Alez Taifa Starz


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.