Ligi Kuu

Tunachohitaji ni ubingwa kwa haraka zaidi- Patrick Aussems.

Sambaza kwa marafiki....

Harakati za Simba kumaliza viporo vyake katika kanda ya Ziwa inaendelea tena leo baada ya kucheza mechi tatu katika ƙanda hiyo na kushinda mechi 6.

Walicheza na Kagera Sugar ya Kagera mechi ambayo walifungwa kwa goli 2-1 . Wakaja kushinda mechi dhidi ya Alliance schools na mechi ya mwisho ni ile waliyoshinda dhidi ya KMC kwa magoli 2-1.

Akizungumza kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems amedai kuwa kwa sasa wanachoangalia ni kupata ubingwa kwa haraka zaidi.


#TimuPWDLGDPts
1Simba SC3829636293
2Yanga SC3827562986
3Azam FC38211253375
4KMC FC38131691555

“Tunahitaji ubingwa kwa haraka zaidi. Tunaenda Mara kwa ajili ya kupata alama tatu ambazo zitatusaidia kupata ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara”.

Akizungumza kuhusiana na ratiba ngumu wanayokabiliana nayo amedai kuwa wamejiandaa kwa hilo.

“Ratiba ni ngumu, ratiba yetu ni mechi , kula ,kulala, safari, mechi tena. Ni jambo gumu lakini tumejiandaa kwa hilo”

Kocha huyo ameonekana kushangazwa na idadi ya mashabiki walioipokea Simba katika mkoa wa Mara.

“Tumepita katika mikoa mingi sana, lakini hatujawahi kuwa na mapokezi makubwa kama haya tuliyoyapata hapa Mara”. Alisema kocha huyo wa mabingwa wa soka Tanzania bara.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.