Shirikisho Afrika

Tuzisahau Milioni 600, tuwaze jua la kesho

Kumbuka: Hatuna hakimiliki ya video hii

Sambaza....

Ndani ya miaka mitatu Yanga imefanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika mara mbili.

Miaka hii mitatu ilikuwa na majira yanayotofautiana kabisa. Nyakati za leo kwa Yanga zina majira magumu sana.

Hapana shaka hali ya uchumi wa Yanga ni mbaya, hakuna pesa nyingi kama kipindi kile walipofanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho chini ya Yusuph Manji.

Leo hii hawana Manji, hakuna anayeweza kuwasimamisha tena , hakuna anayeweza kuwasababisha wakimbie wakiwa na shibe.

Njaa ndilo vazi walilo nalo, vazi ambalo wamelikubali na kulipokea kisha wakalivaa na kukimbia nalo.

Hawaoni soni , kitu cha muhimu kilichopo kichwani mwao ni kupigana kwa ajili ya timu bila kujali magumu wanayopitia.

Wamefanikiwa kufuzu kwenda kwenye hatua ya makundi, unaweza kuwabeza walikutana na timu dhaifu lakini kiuhalisi mpira wa Afrika kwa sasa hauko hivo ndiyo maana Zamaleki ilitolewa na hawa ambao unaweza ukawaona dhaifu.

Image result for YANGA VS WOLAITA DICHA

Kwenye michuano hii ya kimataifa, Yanga imekuwa na wachezaji ambao wanaonekana wa kawaida, lakini ndiyo hao hao ambao wameifikisha timu hapo ilipo.

Leo hii wana Yanga wanayo furaha, na furaha yao ni kupata hizo milioni 600 baada ya kufanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Kuna kitu kichwani mwangu kinaniambia Yanga wanatakiwa watumie nafasi hii kibiashara kuliko kufurahia kuzipata hizo milioni 600.

Kwa namna gani wanaweza wakaitumia nafasi hii kibiashara?

Kuna njia nyingi ambazo mimi nimeziona zina tija kama watu wakiwezekeza akili na muda wao kwenye hizo njia.


Kwenye Masoko (Marketing) four ( 4) Ps kuna vitu vifuatavyo.

Product ( Bidhaa)
Promotion (Matangazo)
Place ( sehemu)
Price ( gharama)


Kufuzu kwa Yanga kwenda katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho viongozi wa Yanga wanatakiwa wachukulie ni Product (bidhaa).

Hakuna kosa kubwa kibiashara kama wakichukulia kufuzu kwao katika hatua ya makundi ya ƙkombe la shirikisho kama kitendo. Wakichukulia kama kitendo ukawaida utakuwepo ndani yao hivo watachukulia vitu kawaida tofauti na kama wakichukulia kama bidhaa hapa mtazamo wa kuchukulia kawaida hautokuwepo.

Baada ya wao kuchukulia kama bidhaa kufuzu kwao katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho wanatakiwa kuwekeza katika kuitangaza bidhaa hii ya kufuzu kwao.

Promotion ( matangazo) yalenge vitu vifuatavyo. Moja kuwafanya mashabiki wa Yanga kuona thamani kubwa ya bidhaa hii, waone ni jambo kubwa na la kujivunia kama shabiki wa Yanga.

Pili, ilenge kujenga wateja loyal wa bidhaa hii, unawaletea bidhaa ya Yanga kufuzu katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika kipi watakipata cha ziada ambacho hakitokuwepo kwenye timu zingine hapa Tanzania?

Wakimaliza hapo, wafikirie kuhusu mkataba wa Macron ambao unaanza rasmi baada ya Yanga kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika. Yanga watavaa jezi zilizotengenezwa na kampuni la Macron na pia Macron watauza jezi hizi.

Image result for Bidhaa za Yanga

Hivo hapa ndipo kuna umuhimu wa ile “P” ya pili yani Promotion (matangazo) , ushawafanya mashabiki wajivunie bidhaa yao ya kufuzu hatua ya makundi na wakawa wateja loyal kwako kinachofuata wekeza msukumo mkubwa katika kuhamasisha ununuzi wa jezi za klabu zitakazouzwa na Macron katika utaratibu mzuri kibiashara ili wazitumie kuja nazo uwanjani.

Yanga wana mechi tatu ( 3 ) za nyumbani katika michuano hii ya kimataifa, hivo wanatakiwa kufikiria kutengeneza mazingira mazuri ya kuuza tiketi na kuwashawishi mashabiki wengi uwanjani.

Mfano wakiwa na kampeni maalumu ya kwenda na Yanga kimataifa, wakawatumia watu maarufu ambao ni mashabiki wa Yanga, wakatumia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari kuhamasisha na kuwahimiza watu kuja uwanjani kwa ajili ya kusafiri na Yanga kimataifa, klabu itapata pesa nyingi kupitia mapato hayo.

Kampeni hii iende sambamba na skafu zenye jumbe mbalimbali za kutia moyo mfano , safiri na Yanga mpaka fainali hii itatia moyo kwa mashabiki na wachezaji wa Yanga kwa kuonesha kuwa lengo la timu ya Yanga siyo kuishia hatua ya makundi peke yake , lengo ni kufika fainali. Umoja huu utaleta madhara chanya kwenye timu ( faida chanya kwenye uchumi wa klabu na matokeo mazuri ya timu ndani ya klabu).

Tukumbuke vyote hivi vitaenda sambamba na Price (gharama) na Place( eneo)

Umeshatambua bidhaa yako (product), ukaifanyia Promotion (matangazo) , unaitafutia sehemu ya kuiuzia kisha unatenga gharama ya kuiuzia ( price).

Gharama za tiketi ziwe ambazo zinaweza kuwafanya watu wa kariba yote kumudu.

Baada ya hapo Yanga wanatakiwa kufikiria kitu kimoja, kipindi hiki wamefika katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Michuano hii itaonekana sehemu kubwa, hivo kuonekana kwa sehemu kubwa kwenye michuano hii inatoa tafasri moja nayo ni kuwa Yanga wametengeneza soko kubwa kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa zao kupitia Yanga.

Hivo basi, Yanga wanatakiwa kukaa chini na kuandaa ushawishi ambao utamwezesha mfanyabiashara aje kutangaza bidhaa yake kupitia jezi ya Yanga.

Hakuna mfanyabiashara asiyependa bidhaa yake itangazwe sehemu kubwa ili kupata wateja wapya na bidhaa yake ijulikane sehemu tofauti, hivo hii ni nafasi ambayo Yanga wanaweza kutumia kuwashawishi wafanya biashara kuja kuwekeza kwao kipindi hiki.

Na hii itafanya kesho yao kuwa bora zaidi kuliko leo yao yenye thamani ya milioni 600

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x