Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa na kocha wa viungo
Shirikisho Afrika

Twende kwa Madiba Tukamsalimie Shakazulu

Sambaza....

Naota ndoto ya kufurahisha, samahanini siyo ndoto nyevu, simuoti Ashura Wala Veronica hapa naota kuhusu Soka la Nchi yangu, tafadhari msinitoe katika ndoto hii waugwana, mnaokula huo ubwabwa pembeni yangu msiniamshe naombeni nyie kuleni tuu mimi nitakula ndoto yanguu.

Tafadhalini mliobize na wapenzi wenu nyie endeeleni tuu si ndo burudani yenu mimi niacheni burudani yangu ni huu usingizi na ndoto yanguu tena mwambieni ex wangu sasa hivi nimejipata na kile kinachonipa furaha.

Naota ndoto Vijana kutoka Jangwani wapo nusu fainali ya CAF Confederation Cup na Vijana kutoka kwa Madiba wamekula chuma mbili kwa mzee wetu hayati Benjamin William Mkapa, nawaona wametanguliza mguu mmoja fainali, ndiyo ni Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na sio fainali ya Mapinduzii Cup ama Azam Sport federation.

Nakurupuka usingizini naikuta ni ndoto ya uhalisia vijana wana kampeni yao ya “Twende kwa Madiba” ndioo twendenii kwa Madiba tukavukie kwenda nusu fainali kulekule kwa mzee Mandela Nelson na Shaka Zulu.

Msikae kinyonge Wananchi jipigeni vifua ni muda wenu sasa, msitetereke, Tp Mazembe alikufa kwake pale Lubumbashi, Rivers akafa kwao pale Nigeria, Club Africain si ndo aliwapa tiketi ya kwenda makundi palepale kwake Tunis, aah ni nani aliyewafunga kwake kwani?, ni yule US Monastrien kwa mabao yake ya ndondokela, let’s go wananchi.

We can’t fear Marrumo twendenii tukamuue palepale kwa Madiba, twende fainali tubebe ndoto kisha turudi Avic town kuendelea kula Ugali na Sukari.

Maendeleo hayana Chama sisi mashabiki wa soka tupo nanyi.

Sambaza....