Sambaza....

Leo hii mwenyekiti wa uchaguzi wa TFF, ametangaza rasmi kusimamisha uchaguzi wa klabu ya Yanga ambao ulipangwa kufanyika tarehe 13/1/2019.

UCHAGUZI YANGA

Hatua hiyo imefikiwa baada ya baadhi ya wanachama wa Yanga katika mikoa ya Dar-es-Salaam, Mbeya na Dodoma kwenda mahakamani kufungua kesi ya kupinga uchaguzi huo.

Pia mwenyekiti huyo wa uchaguzi ametangaza rasmi kusitisha zoezi la kampeni. Tarehe rasmi ya uchaguzi na kampeni itatangazwa jumatatu ijayo.

Sambaza....