BlogLa Liga

Vidal atoa la moyoni, hafurahii kukaa benchi.

Sambaza....

Kiungo Raia wa Chile anayekipiga katika timu ya soka ya Barcelona na nchini Uhispania Arturo Vidal amesema hafurahii kuwekwa benchi katika mechi msimu huu toka ajiunge akitokea Bayern Munich.

Vidal ambaye ameanza katika mechi mbili tu mpaka sasa pamoja na hilo pia amecheza akitokea benchi mara mbili, amesema jambo hilo linamuumiza kwani yeye ni mtu ambaye mara zote amekuwa akipambana kupata namba na muda wa kucheza.

“Nitakuaje na furaha kama sichezi, mimi ni mtu ambaye muda wote nimekuwa nikipambana nikiwa katika timu bora duniani, nimeshinda karibu kila kitu na bado nahitaji kufanya hivyo nikiwa Barcelona,” Jarida ya nchini Chile Diario limemnukuu.

Mara nyingi kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amekuwa akimpanga kiungo wa kibrazil Arthur nafasi ya Vidal katika michezo mingi kwani hata ule mchezo ambao Barca walitoka sare  ya 1-1 na Valencia hakucheza na pia mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Tottenham alicheza kwa dakika tatu tu pekee.

“Kifiziki nipo sawa na nina Furaha, kwa michezo michache iliyopita nimeudhika kidogo, lakini hivyo ndivyo ilivyo, nitaendelea kupambana, bado kuna michezo mingi muhimu kwa timu mbele yetu, tutaona itakavyokuwa,”  Vidal amenukuliwa.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x