Aussems, kocha wa Simba
Ligi Kuu

Waamuzi wetu ni wapuuzi-Kocha wa Simba

Sambaza....

Jana kulikuwa na mechi ya ligi kuu Tanzania bara kati ya Biashara United na Simba iliyofanyika Musoma mkoani Mara.

Mechi ambayo ilimalizika kwa Simba kushinda magoli 2-0 dhidi ya Biashara United ambayo walikuwa wenyeji wa mchezo huo.

Akizungumzia mchezo huo kocha huyo wa Simba amedai kuwa walikuwa wanaenda kukutana na timu ngumu hivo walijiandaa mapema.

“Tulijua Biashara United wana safu imara ya ulinzi, hawajawahi kupoteza mechi chini ya kocha wao huyu”.

“Hivo tulijua tunaenda kukutana na timu ngumu , na tulichotakiwa ni kufunga magoli ya haraka haraka ili mechi isiwe ngumu kwetu”.

Alisema kocha huyo wa Simba ambaye ni raia wa Ubelgiji. Alipoulizwa kuhusiana na kadi nyekundu ya Haruna Niyonzima alidai ni maamuzi ya kipuuzi.

“Kwa wiki za hivi karibuni nimekuwa nikiona maamuzi ya kipuuzi kutoka kwa waamuzi wetu hapa nchini. Hivo huu ni mwendelezo wa maamuzi ya kipuuzi”.

Simba imemaliza mechi zake katika kanda ya ziwa, hivo wanasafiri na kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na kampeni yake ya ligi kuu Tanzania bara.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.