Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la pili lililofungwa na Mo Banka
Ligi

Wachezaji watatu waliobeba YANGA, Tshishimbi BABA LAO !

Sambaza....

 

Nyasi za uwanja wa Taifa zilishuhudia wanaume wawili wakigawana alama moja kwa moja katika mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya magoli mawili , magoli ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere , Deo Kanda huku magoli ya Yanga yalifungwa na Balama Mapinduzi na Mohammed Banka. Hawa ni wachezaji watatu ambao waliobeba Yanga.

PAPY KABAMBA TSHISHIMBI.

Huyu ashawahi kusema yeye ni mchezaji wa mechi kubwa . Mechi kubwa anaweza kukuonesha yeye ni nani . Jana alifanya hivo hasa hasa kipindi cha pili , Baada ya Abdulaziz Makame kutolewa nje na Papy Kabamba Tshishimbi kurudi kama kiungo Wa kuzuia , aliweza kucheza vizuri katikati ya mabeki wa kati na viungo wa kushambulia , alikaba vizuri na kusambaza pasi vizuri katika sehemu ya mbele ya Yanga.

MAPINDUZI BALAMA

Huyu kwangu Mimi alikuwa nyota wa mchezo , alitawala vizuri sana eneo la Kati , alikuwa kiungo bora sana , achana na goli ambalo alilifunga jana , tazama uwezo wake mkubwa wa kusoma mchezo . Umbo zima la kiuchezaji lilitengenezwa na Balama Mapinduzi, yeye ndiye aliyeamua ni jinsi gani Yanga iwe, alipiga pasi vizuri na alirudi nyuma kusaidia kukaba vizuri.

JUMA ABDUL

Baada ya kukaa kwenye majeruhi muda mrefu , alitumia muda mrefu sana kurudi kwenye kiwango chake cha zamani , kiwango ambacho kilimwezesha awe mchezaji bora wa ligi kuu kwa misimu miwili mfululizo. Jana alikuwa kwenye kiwango bora sana , aliweza kukaba na kushambulia mbele.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.