Sambaza....

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza majina yaliyopitishwa kwenye usaili wa Wagombea Uongozi wa Klabu ya Young Africans.
Usaili umefanyika kwa siku 3 Alhamis Novemba 6,2018,Ijumaa Novemba 7,2018 na Jumamosi Novemba 8,2018 Makao Makuu ya TFF Karume,Ilala.
Nafasi ya mwenyekiti Wagombea waliochukuwa na kurudisha fomu walikuwa 3,Wagombea waliopitishwa ni wawili Baraka Igangula na Jonas Tiboroha wakati mgombea Erick Minga ameenguliwa kufuatia taarifa zake alizojaza kwenye fomu kutofautiana na nyaraka halisi.
Nafasi ya Makamu mwenyekiti wagombea waliopitishwa ni 3 Titus Osoro,Pindu Luhoyo na Salum Magege Chota wakati Mgombea mmoja Yoni Kevela ameenguliwa kwa matakwa ya kikatiba baada ya kuchukuwa fomu kugombea nafasi mbili kwa wakati mmoja Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
Nafasi ya Ujumbe waliopitishwa ni Athanas Kazighe,Ramadhan Said,Salim Rupia,Dominic Francis,Shafii Amri,Benjamin Mwakasonda,Christopher Kashiririka,Ally Msigwa,Silvester Haule,Arafat Haji,Frank Kalokole na Said Kambi.
Wagombea Wanne wameshindwa kufika kwenye usaili Hamad Islam,Seko Kongo,Leonard Marango na Benard Mabula kwa mujibu wa kanuni wameenguliwa katika uchaguzi.
Wagombea ambao hawajapitishwa wanayo haki ya kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Sambaza....