Stori

Wanahabari watakataa waondoka na milioni tano

Sambaza....

Timu ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (WANAHABARI FC)wameifunga goli moja kwa bila Timu ya Silent Ocean ukiwa ni mchezo wa utangulizi kabla ya mechi rasmi ya ufunguzi wa Mashindano ya Ramadhani Cup 2023,mchezo huo umefanyika katika Uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jijini Dsm.

Ikumbukwe msimu huu wa Mashindano ya Ramadhani 2023 umedhaminiwa na Simba wa Bahari Silent Ocean Ltd chini ya Mkurugenzi wake Mohamed Soloka ambapo mashindano hayo yanafanyika katika Uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jijini Dsm.

 

Kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari mechi hiyo iliandaliwa ili kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya Silent Ocean Ltd na Waandishi wa Habari za Michezo.

Katika mchezo huo wa kirafiki goli pekee ya Wanahabari FC limefungwa na Pablo Jr akiunganisha mpira ambao ulitemwa na Mlinda Mlango wa Silent Ocean kufuatia shuti lililopigwa na Anuary Binde (Rais wa Takwimu). Kufuatia ushindi huo timu ya Wanahabari FC imejinyakulia kitita cha shilingi milioni 5 za Kitanzania.

Kikosi cha Wanahabari kilichoanza katika mchezo huo.

Walioanza kikosi cha Wanahabari FC:

1.Mwakyoma Jr 2.Richard Kibona 2. Issa Mbuzi 4.Marco Mzumbe 5.Mbwana Mshindo
6.Mselem Kandanda 7.Ibra Digala 8. Ally Kamwe 9.Abdul Mkeyenge 10.Shafii Dauda 11. Anuary Binde [C]

Wachezaji wa Akiba Wanahabari FC:Thobias Sebastian ,James Turpa Turpa, Pablo Jnr, Juma Ayo, Pancreas Bodi ya Ligi, Wilbert Molandi, Dauka Somba, Nassib Mkomwa na Maphoto.

Timu hiyo imara ya Waandishi ilikua chini ya uongozi wa kocha Twalib Muwa, mratibu wa timu Anderson Chicharito na chini ya Waandamizi Charles Abel, Pascal Kabombe na Jacob Mbuya.

 

Sambaza....