Sambaza....

Mashabiki wa Timu ya soka ya Yanga kutoka Tawi la Meatu lililopo wilayani Meatu Mkoani Simiyu  wamesema licha ya baadhi ya Mashabiki kutoka timu pinzani kuwabeza kuwa ni ombaomba wanaamini kikosi hicho kilichopo chini ya kocha raia wa kongo Mwinyi Zahera kitachukua ubingwa wa ligi kuu bara msimu wa Mwaka 2018/19.

Wakitoa salamu za Mwaka Mpya Mashabiki hao wakiongozwa na katibu wao Ramadhani Kamugisha wanasema wamezidi kufurahishwa na matokeo ya kikosi hicho ambacho wanakiita cha Ushindi ambacho mpaka sasa hakijapoteza mchezo hata mmoja.


Ramadhani Kamugisha- Katibu Mashabiki wa Yanga Tawi la Simiyu Meatu

Aidha Mashabiki hao wameuomba Uongozi wa Timu hiyo kutenga muda na kuitembelea wilaya hiyo ili waweze kutoa pongezi zao kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo Mazuri na kujikita kileleni mwa ligi hiyo, Andrew Mzalendo na Charles Dominick ni Mashabiki wa Yanga na wamezungumza na Kandanda.co.tz.

Mashabiki wa Yanga kutoka Simiyu

Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa Mikoa ambayo haina timu hata moja inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara licha ya mashabiki kudai kuwa Simiyu imesheni Vipaji.

Sambaza....