Mataifa Afrika

Wapinzani wa Simba kutua nchini Jumatatu.

Sambaza....

Simba watakua nyumbani kuikaribisha Vipers ya Uganda katika mchezo wa Kundi C wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kumaliza kibarua chake cha michuano ya kombe la FA dhidi ya African Sports.

Simba wanakwenda kutupa karata yao ya nne katika kundi lao ambapo msimamo wa kundi unaonyesha bado wana nafasi wakiwa na alama zao tatu huku wapinzani wao Vipers wakiwa na alama moja pekee.

 

Kuelekea mchezo huo utakaopigwa siku ya Jumanne Marchi saba katika Dimba la Benjamin Mkapa Vipers wao wamesema wanakuta nchini siku ya Jumatatu asubuhi taarifa ikitolewa na Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally.

“Wageni wetu Vipers watafika nchini siku ya Jumatatu asubuhi. Lakini pia waamuzi watafika nchini Tanzania Marchi tano wakitokea Ethiopia,” alisema Ahmed.

Simba mpaka sasa wanashika nafasi ya tatu katika kundi lao na ili wafufue matumaini yao yakufuzu kuelekea robo fainali ni lazima wapate ushindi katika mchezo huo wa nyumbani. 

Katika mchezo wa awali wawilo hao walipokutana Uganda Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja bila lililofungwa na Henock Inonga Baka.

Sambaza....