Blog

Wiki ya Mwananchi yatua Kitunda leo

Sambaza kwa marafiki....

Tawi la yanga kitunda likiwa katika wiki ya Mwananchi leo limekamilisha shuguli za kijamii kwa kufanya usafi Hospitali ya kitunda,Polisi Kitunda,Ofisi ya serikali ya Mtaa Kitunda na Kituo cha watoto Yatima Kipunguni ambapo walikabidhi vyakula,Ndoo za maji,Mifagio ,sabuni na Pesa taslimu.

Matukio haya yote yanayoendelea nchini kwa mashabiki wa Yanga ni kwaajili ya kuelekea katika kilele cha wiki ya mwananchi ambayo lengo lake litakuwa kuwatambulisha wachezaji wake na mambo mengine kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.