Dickson Ambundo akiwa na kikosi cha Alliance fc.
Ligi Kuu

Yanga imuwahi AMBUNDO kabla hajawa GHALI

Sambaza....

Yanga ilianza kuishi leo tangu zamani, ilianza kuishi kwenye dunia ya mpira wa kisasa tangu zamani, kwa kifupi zamani ilikuwa inaishi kwenye dunia ambayo kwa sasa ndiyo tunaishi.

Dunia ambayo mshambuliaji wa kati hana thamani kubwa sana ukilinganisha na mshambuliaji ambaye hufunga magoli na kutoa pasi za mwisho akitokea pembeni.

Dunia ambayo washambuliaji wa kati hawana umuhimu sana kwa sababu tu ya hawa viumbe ambao wana uwezo wa kufunga na kutoa pasi za mwisho wakitokea pembeni.

Ni viumbe hawa hawa ambao wanahatarisha maisha ya washambuliaji wa kati. Siku hizi ni wachache sana, sijui wameenda wapi, kwa kifupi wanapotea kwa kasi sana.

Na watu hawashtuki kupotea kwao kwa sababu hakuna pengo ambalo wanalipata. Real Madrid hawakuwa na lawama kwa kupotea kwa watu kama Ronaldo De Lima kwa sababu walimpata Cristiano Ronaldo.

Hawa watu ndiyo wanaoitawala dunia ya mpira kwa sasa, na ndiyo wana thamani kubwa sana kwenye dunia ya mpira wa sasa.

Na ndiyo kila jicho huwatazama, makocha hutamani kuwa nao kwenye kikosi, mashabiki hutamani kuvaa jezi zenye namba zao na hata makampuni ya kibiashara hutamani kuwapa mikataba minono ya kibiashara.

Huwezi kupata hasara kwa hawa watu kwa sababu ni vipenzi vya wengi. Muda mwingi hutumia kuwafurahisha mashabiki wao.

Muda mwingi hutumia kuibeba timu yao, ndiyo maana Leo hii Mbappe ni muhimu zaidi ya Cavann, inawezekana Cavann anafunga sana lakini hatazamiki kwa umuhimu mkubwa kama Mbappe.

Mtu ambaye anafunga na kutoa pasi nyingi za magoli tena mbaya zaidi akitokea katika eneo ambalo siyo la karibu na goli ukilinganisha na Cavani.

Haya ndiyo maisha ya sasa ya mpira, ndiyo tunayoyaishi na tumeyachagua kwa kuyaamini ni bora zaidi kuliko maisha ya zamani.

Ndiyo maana tunatunga mashairi mengi sana kuwatukuza watu kama kina Neymar, na kuwasifu watu kama kina Ousmane Dembele.

Kwa sababu tu hawa ndiyo huleta utukufu katika dunia yetu ya kisasa ya mpira. Dunia ambayo ni ngumu kuikwepa kabisa.

Dunia ambayo wenzetu Yanga walianza kuishi kwa muda mrefu sana. Yanga kwa muda sana hawajawahi kumtegemea sana mshambuliaji wa kati.

Ni msimu huu na msimu uliopita ndiyo wameanza sana kuwategemea washambuliaji wa kati. Msimu jana zilihitajika juhudi za Obrey Chirwa kuibeba Yanga lakini haikufika popote.

Msimu huu kila mwana Yanga anategemea miguu ya Makambo katika ufungaji wa magoli. Huyu ndiye mfungaji wao bora mpaka sasa.

Kwa kifupi huyu ndiye anawabeba sana na ndiye mwenye thamani kubwa kwa sasa ndani ya kikosi cha Yanga. Kitu ambacho hakikuwepo kipindi cha nyuma.

Kipindi cha nyuma Yanga ilikuwa inawategemea sana wachezaji ambao walikuwa wanacheza pembeni. Hawa ndiyo walikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga na kutoa pasi za mwisho.

Masikio yangu yalianza kupevuka kimpira kwa kuanza kumsikia Edibily Lunyamila. Mchezaji bora wa Yanga.

Huwezi kutaja kikosi bora cha wakati wote cha Yanga bila kumtaja Edibily Lunyamila. Hakuwa mshambuliaji wa kati.

Alikuwa anatokea pembeni mwa uwanja, alifunga magoli na kutoa pasi za mwisho nyingi akitokea pembeni. Baada ya Edibily Lunyamila alikuja Said Maulid.

Huyu naye alikuwa anafanya kile kile ambacho Lunyamila alikuwa anakifanya kipindi chake. Mrisho Ngassa ndiye alikuja kuwa lulu.

Huyu alikuwa mchezaji mwenye thamani kubwa sana. Na alikuwa mchezaji mwenye kipaji kikubwa sana ambacho hakikufika sehemu kubwa.

Tuachane na hii mada , ni mada ya siku nyingine. Turudi kwenye mada yetu. Mrisho Ngassa alifunga sana akitokea pembeni.

Na inasemekana ndiye mfungaji bora wa wakati wote wa timu ya taifa ya Tanzania bara. Magoli ambayo aliyapata akitokea katika eneo la pembeni mwa uwanja.

Dickson Ambundo

Ngao ya Jamii

MsimuTimu
Jumla-

TPL

MsimuTimu
2020-2021Dodoma FC0000000
Jumla-0000000

Alipoondoka yeye alikuja Simon Msuva, huyu naye alikuwa na sifa zile zile za kina Ngassa. Alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu mara mbili akitokea pembeni mwa uwanja.

Alikuwa na thamani kubwa sana, lakini baada ya yeye kuondoka Yanga walikosa mtu ambaye anaweza kuishi kwenye dunia yao , dunia ya kisasa.

Dunia ambayo kwa sasa watu wengi wanaishi, dunia ambayo wachezaji wanaotokea pembeni mwa uwanja wanahitajika sana.

Lakini kuna kitu kimoja ambacho Yanga nimetamani kuwakumbusha na kuwauma sikio tu kwa wema. Pale Alliance FC kuna kijana anaitwa Dickson Ambundo.

Mchezaji ambaye msimu jana kwenye ligi daraja la kwanza alikuwa mfungaji bora akiwa na magoli 11. Msimu huu kwenye ligi kuu ya Tanzania bara amefunga magoli 7, magoli manne nyuma kufikia idadi ya magoli yake msimu Jana.

Hapo msimu haujaisha, bado unaendelea na anakimbizana vizuri kwenye kiatu cha ufungaji bora. Huyu siyo mshambuliaji wa kati bali anatokea pembeni.

Ni aina ya wachezaji ambao Yanga huwatumia sana kwa kipindi kirefu na kwa kipindi hiki wamepotea kwenye kikosi cha Yanga. Ana kipaji kikubwa sana, ni moja ya vijana ambao wakipewa nafasi kubwa wanafanya makubwa, ni vyema Yanga wamuwahi kabla hawajawa wa gharama.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x