Benchi la ufundi la Yanga!
Stori

Yanga Kamili Kutua Tanga Kutetea Taji Lao

Sambaza....

Wananchi Yanga wanaondoka Jijini Dar es salaam leo na kuelekea mkoani Tanga tayari kabisa kwenda kushiriki michezo ya Ngao ya Jamii katika Dimba la Mkwakwani.

Yanga wataondoka na ndege siku ya leo na kutua Tanga ambapo watapumzika na kufanya mazoezi kesho Jumanne na Jumatano watakua dimbani kumenyana na Azam Fc katika mchezo wakwanza wa Ngao ya Jamii.

Kwa msimu huu Ngao ya Jamii inachezwa kwa mtindo tofauti ambapo imezishirikisha timu nne na si mbili kama ambavyo imekua ikichezwa awali miaka yote.

Kama Wananchi watapa matokea ya ushindi katika mchezo huo utakaopigwa Jumatano usiku basi watakwenda fainali na kumsubiri mshindi kati ya Singida Fointaine Gate au Simba watakaocheza Alhamis usiku pia.

Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini.

Fainali za Ngao ya Jamii zinatarajiwa kupigwa Augusti 13 hapohapo Mkwakwani Tanga wakati pia watakaofungwa watacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu siku hiyohiyo saa tisa alasiri.

Ikumbukwe Yanga ndio watetezi wa Ngao hiyo kwani mwaka jana walifanikiwa kuitwaa kwa kuifunga Simba mabao mawili kwa moja katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Sambaza....