Ligi

Yanga kucheza Matopeni tena

Sambaza....

Baada ya mechi iliyopita dhidi ya Mbeya City kocha wa muda wa Yanga , Charles Boniface Mkwasa kulalamika hali ya uwanja wa Sokoine Mbeya kuwa na hali Mbaya kutokana na mvua kubwa kunyesha, hali ya Uwanja huo inazidi kuwa Mbaya kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Prisons.

Jana kulikuwa na Show ya Rayvanny msanii kutoka label ya Wasafi Classic Baby (WCB) kwenye uwanja huo wa Sokoine Mbeya , show ambayo ilihudhuliwa na watu wengi na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye uwanja huo.

Hali ya nyasi za uwanja wa Sokoine kwa sasa ni Mbaya Sana na inazidi kuwaweka Yanga katika nyakati ngumu katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Prisons na unaweza kuwagharimu kucheza tena matopeni.

 

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.