Ligi Kuu

YANGA ni tishio, Simba timu ya kawaida-MKWASA

Sambaza....

Jana Yanga ilikuwa na mechi kwenye uwanja wa uhuru, mechi ambayo ilishuhudia Yanga wakishinda magoli 4-0, magoli yaliyofungwa na Papy Kabamba Tshishimbi, Patrick Sibomana , Lamine Moro na David Molinga.

Baada ya mechi hiyo ambayo I lishuhudiwa nyuki wakivamia eneo la kuchezea ndani ya uwanja, kocha wa muda wa klabu hiyo Boniface Charles Mkwasa amedai kuwa kwa sasa Yanga inaimlika.

“Maelekezo tunayowapa mazoezini kwa sasa wanayaonesha uwanjani , timu inazidi kuimarika kila Siku , ndiyo maana unaona timu inafunga magoli 4 kitu ambacho mwanzoni hakikuwepo”-alisema Mkwasa.

Alipoulizwa kuhusu mechi ya Simba na Yanga , Charles Mkwasa amedai kuwa kwa sasa lengo lao siyo mechi ya Simba wanatazama mechi za viporo ambazo zipo mbeleni kwao.

“Kwa sasa lengo letu siyo mechi ya Simba , tunazitazama mechi za viporo ambazo zipo usoni kwetu , Simba ni timu ya kawaida kama timu zingine” alimalizia kwa kusema hivo kocha huyo ambaye anauzoefu mkubwa kwenye soka la Tanzania.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.