Blog

Mambo mazuri yanakuja Yanga

Sambaza....

Klabu ya Yanga tayari imeshaitisha mkutano wa dharula chini ya mwenyekiti wao Mshindo Msolla ambao utafanyika mwezi ujao (Februari). Moja ya ajenda za mkutano huo ni mabadiliko ya Katiba yao ili iweze kuendana na yale ambayo inataka kufanya. Tazama Katiba yao ilivyo na mapendekezo wanayoyataka.

Ilivyo..

Ibara ya 7(1) Mtu anayetaka kuwa mwanachama atawasilisha maombi ya uanachama kwa Katibu wa tawi ili yajadiliwe na kamati ya tawi.j

Mapendekezo

Ibara ya 7(1) (a) Mtu anayetaka kuwa mwanachama atawasilisha maombi ya uanachama kwa Katibu wa tawi ili yajadiliwe na kamati kuu ya tawi.
Ibara ya 7(1) (b) Kutakua na Wanachama ambao wamesajiliwa kwa mfumo wa kielectroniki na watatambulika kuwa wanachama halali kwa mujibu wa katiba.

Ilivyo…

Ibara 7(3) Maombi yataambatanishwa na:
a) Fomu ya Maombi ( Fomu Na.
YASC/U/1) iliyojazwa ipasanyo;
b) Ada ya uanachama ambayo ni shs.
12,000 kwa mwaka.
c) Ada nyingine yoyote
itakavyoamuliwa na Young Africans Sports Club. Miongoni mwa ada hizo ni shs. 1,000/- kama gharama ya fomu na shs. 2,000/- ambayo ni gharama ya kadi.
d) Tamko linalosema kwamba anakubali kufuata sharia hizi, kanuni na maagizo katika muundo wake wa sasa, na kutegemea mabadiliko ya baadaye na pia maamuzi ya IDFA, DRFA, TFF pamoja na ligi zinazoundwa na vyama hivyo;
e) Tamko linalosema kwamba anatambua mamlaka ya pekee ya Baraza la Usuluhishi kuhusiana na migogoro yote ya kisheria inayohusu masuala ya mpira wa miguu.

Mapendekezo..

Ibara ya 7(3) Maombi ya Uanachama yatafanyika kwa njia ya ki electroniki.
a) Ada ya uanachama ambayo ni Sh. 1500 kwa mwezi.
b) Ada nyingine yoyote kama itakavyoamuliwa na Young Africans Sports Club. Miongoni mwa Ada izo ni shs. 2000 kama gharama ya kununua fomu kielectroniki na Shs. 10,000 ambayo ni gharama ya kadi, lakini bila kuathili malengo ya kipengele hiki, Sekretarieti inaweza kuweka ada ya madaraja ya uanachama kama itakavyoona inafaa kwa idhini ya Kamati ya Utendaji ya Young Africans Sports Club.

c) Tamko linalosema kwamba anakubali kufuata sharia hizi, kanuni na maagizo katika muundo wake wa sasa, na kutegemea mabadiliko ya baadaye na pia maamuzi ya vyama vya soka kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa mpaka Taifa pamoja na ligi zinazoundwa na vyama hivyo.
d) Tamko linalosema kwamba anatambua mamlaka pekee ya kuamua kuhusu mwanachama ikiwa ni pamoja na kumfukuza uanachama.

Ilivyo…

Ibara ya 62: Matawi ya Klabu

  1. Kutakuwepo na matawi ya wanachama katika maeneo
    mbalimbali hapa nchini nan je ya nchi kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 6 ya Katiba hii. Kiwango cha chini cha idadi ya wanachama ambao wanaweza kuunda tawi kisipungue watu mia moja (100).
  2. Uanzishwaji wa Tawi utaidhinishwa na Kamati ya Utendaji baada ya kupitia maombi ya uanzishwaji huo yaliyowasilishwa kwa Katibu Mkuu na ambaye ndiye atakayewasilisha kwa Kamati ya Utendaji ili iyajadili na kuidhinisha au kuyakataa kwa kutoa maelekezo yanayostahil.
  3. Kutakuwa na uongozi wa ngazi ya matawi utakaochaguliwa na wanachama wa Tawi husika. Viongozi wa tawi watakaochaguliwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka hazina na wajumbe wa tawi wasiozidi wane.
  4. Katibu wa tawi anawajibiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu orodha ya viongozi waliochaguliwa katika tawi husika.-
  5. Wajibu wa kila tawi ni kutoa ushauri kwa Kamati ya Utendaji kwa kupitia Katibu Mkuu kuhusu masualambalimbali kwa manufaa ya Klabu. Miongoni mwa masuala hayo ushauri katika kubuni mikakati mbalimbali ya kuisaidia Klabu kiuchumi na kuleta ushindi kwa timu katika michuano mbalimbali. Aidha tawi ni kiungo muhimu kati ya uongozi na wanachama popote pale walipo.
  6. Matawi yanaweza kuunda Kamati ambacho kitakuwa ni chombo cha kuishauri Kamati ya Utendaji katima masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kuleta ushindi kwa timu katika michuano mbalimbali.
Mapendekezo ya Kandanda

Mapendekezo..

Ibara ya 62 iongezewe kifungu cha 7 kisomeke hivi:
Uanzishwaji wa Tawi utaidhinishwa na Kamati ya Utendaji baada ya kupitia maombi ya uanzishwaji huo yaliyowasilishwa kwa Katibu Mkuu kupitia mfumo wa kielectroniki na ndiye atakayewasilisha kwa kamati ya utendaji ili iyajadili na kuidhinisha au kuyakataa kwa kutoa maelekezo yanayostahili.

7. Kutakua na Uongozi wa ngazi ya Wilaya na Mkoa ambao watakua ni wawakilishi wa Klabu katika maeneo husika na watachaguliwa kwa utaratibu ufuatao:-
i) Viongozi wa Wilaya watachaguliwa miongoni wa Wenyeviti wa Matawi ndani ya Wilaya husika ambao watatambulika kama
wenyeviti wa wilaya.
ii) Viongozi wa Mkoa watachaguliwa miongoni mwa Wenyeviti wa wilaya ambao watatambulika kama wenyeviti wa mikoa.

iii) Wajumbe watapashwa kuchagua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, na Muweka hazina.

iv) Katika kuchagua viongozi wa wilaya wajumbe muhutasali vilivyowachagua hao pamoja na majina ya viongozi waliochaguliwa na vyote vitatumwa kwa Katibu Mkuu.

v) Viongozi wote wa Mkoa, Wilaya, na Matawi watakua ni wawakilishi wa Young Africans Sports Club katika maeneo husika na watawajibika moja kwa moja kwa Katibu Mkuu.

vi) Viongozi wote watahudumu kwa mda wa miaka miwili japo wanaweza kugombea tena.

Sambaza....