Mashabiki wa Klabu ya Yanga
Stori

Yanga: Wiki ya Mwananchi ni Mwanza

Sambaza....

Rasmi klabu ya soka ya Yanga kupitia msemaji wake Alli Kamwe wamesema Wiki ya Mwananchi itaanzia mkoani Mwanza kwa mara ya kwanza.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Alli Kamwe alisema “Mwaka huu kickoff rasmi ya Wiki ya Mwanachi itakua mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha,” alisema na kuongeza “Tunakwenda Mwanza kuonyesha ukubwa wa Yanga hivyo mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga waje wajitokoze kwa wingi.”

Alli Kamwe sambamba na kutangaza viingilio lakini pia alisema Wananchi wa Mwanza watapa fursa ya kupiga picha na makombe yao matatu.

Mataji ya Yanga 2022-2023.

“Mataji yetu yote matatu tuliyoshinda msimu uliopita yatapanda ndege na mashabiki watapa fursa yakupiga nayo picha. Hapa mashabiki waliojiandikisha na kujisajili na kadi ya CRDB ndio watakaopata fursa hiyo.”

Yanga pia wametangaza viingilio vya siku ya Wananchi ambapo mzunguko ni Tshs 10,000, VIP C ni Tshs 30,000 na 20,000, VIP B Tshs 40,000, VIP A ni Tshs 100,00 na Royal ni Tshs 300,000, wakati VVIP ni 500,000.

Sambaza....